MWANZO|USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANO DeutschEnglishKisuaheli

Daktari kutoka Tirol anayetoa huduma katika hospitali ya Mt. Fransisko

12/05/10 - 27/08/2010
Mwanaushirika wetu Dr. Franz Josef Wilhelm, Mganga kutoka Oetz/ Tirol alifanya maamuzi baada ya kustaafu kwake, kutumia ujuzi na uzoefu wake wa wahanga wa moto, kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa wa hospitali ya Mt. Fransisko.

Katika kipindi kifupi cha kujipatia uzoefu katika idara ya wagonjwa wanaofika hospitali kupata matibabu na kisha kurejea makwao, aliweza kujielimisha kwa kiasi kikubwa juu ya magonjwa ki – tropiki ambayo kwa kawaida wazungu hawayafahamu.

Katika majuma na miezi iliyofuata, Franz Josef alianza kufanya kazi kwenye chumba cha tatu ( 3 ) cha upasuaji ambako kwa kawaida majeruhi wa aina mbalimbali hutibiwa. Mbali na kuvunjika kwa mifupa kama vile mkono na mguu ambayo ni kawaida hata Ulaya, ajali zitokanazo na kuumwa na wanyama kama vile mamba, kiboko na nyani ni changamoto kubwa.