MWANZO|USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANODeutschEnglishKisuaheli

Madaktari kwa ajili ya Ifakara

Msaada kwa lengo la kujitegemeza - Mradi wa ki-austria, "Tiroli", katika kiini cha Africa

Ushirika wa „Madaktari kwa ajili ya Ifakara“ umeanzishwa kwa lengo la kuisaidia hospitali ya Mtakatifu Fransisi ambayo ni hospitali teule ya wilaya. Hospitali hii ambayo iko katika mji wa Ifakara, kusini mashariki mwa Tanzania, ilianzishwa na shirika la wakapuchini toka nchini Uswisi kwa kushirikiana na daktari mtaalam wa upasuaji, Dk. Karl Schöpf kutoka nchini Austria, ambaye kwa sasa anaishi Zams, Tiroli – Austria.

Kwa kushirikiana na shirika la „msaada wa kimaendeleo“ la Austria, serikali ngazi ya mkoa wa Tiroli na watu wengi binafsi tunaelekeza jitihada zetu katika kuboresha kiwango cha matibabu katika sehemu mahalia.

Wanakikundi si tu madaktari bali pia watu kutoka taasisi nyingine na makundi mbalimbali ya wataalamu ambayo yanausaidia umoja wetu kwa jitihada kubwa: hawa ni pamoja na wauguzi, wachoraji, mafundi, watumishi wa serikali, wafanyabiashara, shule na wengine wengi.

 Siku za dharura Längenfeld 2017
10.06.2017
Waandaaji walitupatia nafasi ya kuutambulisha ushirika wetu.
habari zaidi
 Tanzania Training Centre for International Health (TTCIH)
Tafadhali tembelea tovuti ya Tanzanian Training Centre for International Health in Ifakara
http://www.ttcih.org/
 Harambee iliyofanywa na Shule ya Wauguzi Reutte, Austria
5.4.2017
Chuo cha Wauguzi kilichopo Reutte nchini Austria kilisherehekea Mahafali ya shahada ya Uuguzi na kufanya harambee kuichangia Hospitali ya Rufaa ya Mt. Fransisko, Ifakara.

Soma zaidi>>>>

Page: 1 of 6 | Hits: 1 to 3 of 18 |