MWANZO|USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANO DeutschEnglishKisuaheli

Ifakara limekuwa jimbo katoliki

Tarehe 14.01.2012, "siku ya Afrika ulimwenguni" Baba Mtakatifu Benedikto XVI ameitangaza wilaya ya Kilombero kuwa jimbo jipya la "Ifakara".

Lililokuwa jimbo la Mahenge sasa limegawanywa katika majimbo ya Mahenge ( sasa likiwa na wilaya moja tu ya Ulanga) makao makuu yake yakiwa Mahenge na likiendelea kuongozwa na Mhashamu Askofu Agapiti Ndorobo, na jimbo jipya la Ifakara ( linaloundwa na wilaya ya Kilombero) makao makuu yake yakiwa Ifakara.

Askofu wa kwanza katika jimbo hili jipya ni Mhashamu Salutaris Libena, ambaye amekuwa Askofu msaidizi katika Jimbo kuu la Dar-es- Salaam. Mhashamu Salutaris anatokea Ifakara ambako baba yake alikuwa mwalimu.
Kwa tendo hili mji wa Ifakara umeongezewa umaarufu wake; Sasa ni mji wenye chuo kikuu na pia ni makao makuu ya Jimbo.

Mhashamu Askofu Agapiti Ndorobo anaendelea kuwa Askofu wa Jimbo la Mahenge (lililopunguzwa ukubwa wake) na makao makuu yakiwa Mahenge - Kwiro