MWANZO|USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANO DeutschEnglishKisuaheli

Safari ya majifunzo ya Dr. Rashid Mayoka katika mji wa Salzburg nchini Austria .

November 2010
Dr. Rashidi Mayoka, Mkuu wa Idaya ya Upasuaji katika Hospitali ya Mt. Fransisko alikuwa nchini Austria katika mji wa Salzburg kwa majuma manne. Huko alikuwa katika hospitali ijulikanayo kama "Krankenhaus der Barmherzigen Brüder" akichukua mafunzo ya ‘Endoscopy’.

Haya ni majifunzo ya matumizi ya chombo katika huduma ya upasuaji, chombo chenye mrija au bomba ndefu inayoingizwa katika mfumo wa chakula na kuonesha hali ya ndani ya mwili wa binadamu. Wenyeji wa Dr. Mayoka walikuwa Profesa Dr. Klaus Schwamberger aliyekuwa zamani mkuu wa idara ya upasuaji katika hospitali ya "Krankenhaus der Barmherzigen Brüder" pamoja na Dr. Gerhard Kunit aliyekuw zamani mkuu wa idara ya ‘Urology’-tiba ya mfumo wa haja ndogo kwa binadamu. Shukrani nyingi ziende kwa Dr. Helmut Weiss ambaye kwa ukarimu wake amemwesha Dr. Mayoka kuongeza ujuzi katika maeneo yafuatayo: ‘gastroscopy’ na ‘coloscopy’ -uchunguzi wa hali ya tumboni mwa binadamu kwa kutumia kifaa maalumu; pamoja na ‘cystoscopy’ -uchuguzi wa njia ya mkojo. Umoja wa Madaktari Rafiki wa Ifakara wamegharimia upatikanaji wa vifaa vitavyo muwezesha huduma katika maeneo hayo zitolewe kwa wagonjwa katika hospitali ya Ifakara.