Mashine mpya ya Mionzi (X-ray) kwa ajili ya Hospitali ya Mt. Fransisko
Mashine ya zamani ya mionzi ilihitaji matengenezo ya mara kwa mara. Hatimaye, mashine hiyo ikaharibika kabisa.

Katika picha ni Bwana Prashant Gokarn toka Kampuni ya Vanguard na fundi wake. Wengine ni Christine Schennach na Godfrey Mkwiche
Umoja wa Madaktari kwa ajili ya Ifakara kwa kushirikiana na uongozi wa hospitaliu metatua tatizo hilo kwa kununua mtambo mpya wa mionzi aina ya Multix Swing uliotengezwa na kampuni ya Siemens ya Ujerumani. Mashine hiyo imeundwa kwa kuzingatia mahitaji ya nchi za ki tropiki. Kampuni ya Vanguard inayoongozwa na Bwana Prashant ambayo ina makao yake mjini Dar es Salaam, itahusika na matengenezo ya mashine hiyo pindi itakapohitajika.

Mgonjwa wa kwanza akipata huduma

Dk. Anthony Bw. Helmut Suitner, mwakilishi wa Serikali ya Austria, Mhashamu Askofu Agapiti Ndorobo wakielekea kwenye sherehe ya ufunguzi


