Agosti 2010-Mtambo wa kufua Umeme wa Jua katika Hospitali ya Mt. Fransisko .
Gharama za umeme ambazo hospitali imekuwa ikipata iwe ni kutoka TANESCO au kwa matumizi ya Generator imekuwa ikipanda sana .

Pichani ni Alexander Zangerle na Godfrey Mkwiche wakipanga namna ya kufunga mitambo ya Umeme Jua
Maeneo ya hospitali yanayotumia umeme kwa wingi ni pamoja na mitambo ya kupoozesha hewa katika Chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) na mitambo ya kuchemsha maji katika sehemu ya kufulia nguo (Laundry). Mipango imefanywa ili kwamba maeneo haya yatumie umeme unaotokana na Jua, hii itapunguza matumizi ya umeme hospitalini kwa asilimia ishirini na tano.

Timu ya wataalamu wafunga mitambo


