MWANZO|USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANO DeutschEnglishKisuaheli

2010 - Maji Safi na salama kwa matumizi ya Hospitali ya Rufaa ya Mt. Fransisko Ifakara.

Hospitali ya Mt. Fransisko inapata huduma ya maji toka visima vya zamani ambavyo kwa sasa havitoi maji ya kutosha. Mara kadhaa maji yamekosekana hospitalini.

Uzio kwa ajili ya usalama


Kufuatia maombi toka hospitalini, Umoja wa Madaktari Rafiki wa Ifakara pamoja na Uongozi wa Hospitali uliazimia kugharimia uchimbaji wa kisima kipya cha maji. Kampuni ya uchimbaji visima toka Dar es Salaam ilifanikisha uchimbaji wa kisima cha mpaka kina cha mita 100 kwa muda mfupi sana . Timu ya wataalamu toka hospitalini ikashughulikia ufungaji wa mashine ya kuvuta maji, kuweka uzio, kufunga mabomba ya kusambaza maji toka kisimani hadi hospitalini pamoja na kufunga mitambo ya umeme kama ilivyohitajika.

Kisima hiki kipya kinatoa sasa lita 18,000 za maji safi na salama kwa saa, hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo kubwa la kukosa maji ya kutosha hospitalini. Hata hivyo shughuli kubwa iliyo mbele yetu ni kuhakikisha visima vitatu vya zamani vinafanyiwa ukarabati.