MWANZO|USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANO DeutschEnglishKisuaheli

Maji kwaajili ya hospitali ya Mt. Fransisko

5.12.2011
Katika siku hii unaanza mradi mkubwa utakaohakikisha maji yanasambazwa katika hospitali ya Mt. Fransisko.
Tunawaomba wote kusaidia mradi huu muhimu na wa haraka

Hakuna utakaswaji wa vifaa vya hospitali pasipo maji

Katika miezi na miaka iliyopita, hali ya upatikanaji wa maji katika hospitali ya Mt. Fransisko imezidi kuzorota. Wakati fulani maji hukatika mapema muda wa mchana na mara nyingi maji hukatika kwa kipindi kirefu. Kitendo hiki kinamaanisha nini katika hospitali kubwa kama hii, haihitaji maelezo zaidi. Mfumo wa maji uliopo sasa hivi ni ule wa tangu miaka ya 50, kwa sasa hivi umezeeka na kuchakaa. Kwa nyongeza ni kwamba, idadi ya watumiaji wa maji inaongezeka zaidi na zaidi. Miongoni mwao ni chuo kikuu kipya chenye ongezeko la wanachuo na wahadhili, chuo cha wauguzi na taasisi nyingine nyingi.

Moja kati ya matenki mawili, yenye ujazo wa lita 50,000 likiwa bado katika harakati za ujenzi.


Hivyo, ushirika wetu umeamua kufanya ukarabati ili kuhakikisha maji safi yanasambazwa kwa muda usiopungua miaka 10.
Hatua za ujenzi zitachukua takribani miezi 3.

Ufafanuzi wa mradi
Gharama za mradi