MWANZO|USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANO DeutschEnglishKisuaheli

St. Francis University College of Health and Allied Sciences (SFUCHAS)

Kwa miaka kadhaa sasa zitihada zimekuwa zikifanyika kuiendeleza hospitali ya Mt. Fransisko kuwa tawi la chuo kikuu cha Mt. Agustino Mwanza kitivo cha utabibu. Habari njema ni kwamba jitihada hizi hatimaye zimezaa matunda. Tarehe 1.12.2010 Mhashamu Askofu Agapiti Ndorobo aliadhimisha misa maalum kufuatia kupandishwa hadhi kwa hospitali hii kuwa chuo kikuu kinachoshughulikia afya na michepuo yake.
„St. Francis University College of Health and allied Sciences", (SFUCHAS)
Tendo hili ni muhimu sana kwa serikali ya Tanzania, maana tawi hili jipya la chuo kikuu litasaidia kwa hakika kupunguza tatizo kubwa la upungufu mkubwa wa madaktari uliopo nchini. Wakati huo huo itakuwa changamoto kubwa kwa hospitali na jimbo la Ifakara.

Kiungo kwenye tovuti ya SFUCHAS