MWANZO|USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANO DeutschEnglishKisuaheli

Kampeni ya Hisani "Africa shopping bags" ya kampuni ya MPreis

MPreis ni Kampuni inayoshughulika na biashara ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali. Wateja huhitaji mifuko kwa kuwekea bidhaa wanazonunua. Mwaka huu pia Kampuni imekubali kutengeneza mifuko ambayo itauzwa kuchangia mahitaji ya umoja wetu. Kwa ukarimu wa wateja, takribani mifuko 300,000 iliuzwa mwaka uliopita na kukusanya Euro 40,000 kwa umoja wetu.

Pichani ni Mag. Ingrid Heinz na Dk. Wilfried Schennach

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mag. Anton Moelk.art, Michaela Schweeger na Mag. Ingrid Heinz kwa utayari wao wa kutoa msaada kwa ajili ya kusaidia kazi zetu katika hospitali ya Ifakara. Kwa ombi rasmi la Mag. Anton Moelk, fedha zilizokusanywa zinapaswa kutumika kulipia gharama za mafunzo kwa watumishi na hasa kuinua kiwango cha taaluma ya madaktari kuwa madaktari bingwa