USHIRIKA|TANZANIA|MAWASILIANODeutschEnglish

Hospitali ya rufaa ya Mt. Fransisko

Hospitali ya Mt.Fransisko ni mali ya jimbo katholiki la Mahenge. Kufuatia mtataba wake na serikali, hadi hivi karibuni hospitali hii imekuwa ikitoa huduma kama hospitali ya wilaya. Iliwajibika kutoa huduma ya tiba kwa wilaya za Kilombero na Ulanga eneo lenye takribani wakazi 600,000 na lenye ukubwa karibu sawa na nchi ya Uswisi. Tarehe 28.06.2010 waziri wa afya Prof. David Mwakyusa aliitaja rasmi hospitali ya Mt. Fransisko kuwa hospitali ya rufaa. Hivi inakuwa moja kati ya hospitali tisa (9) za rufaa nchini Tanzania. Hii inamaanisha kuwa, hospitali zote za wilaya zinazozunguka eneo hili zisizokuwa na vifaa na wataalamu wa kutosha na hivyo kutoweza kuwatibu wagonjwa kadhaa ipasavyo, zitakuwa zikiwahamisha kwenda Ifakara. Uwanja wake wa kazi umepanuliwa kwa namna hii na waganga na wauguzi wake sasa wanakabiliwa na changamoto mpya na kubwa.

Ilijengwa kwa kufuata viwango vya Ulaya

Picha ya hospitali ya Mt. Fransisko kama ilivyopigwa kutoka kwenye ndege Jengo la hospitali mpya lilisanifiwa.na Dr. Karl Schöpf mwenyewe. Alinuia kujenga hospitali ya kisasa yenye kiwango sawa na zile za Ulaya. Hivyo usanifu wake umezingatia hali ya hewa ya kitropiki, ina mwanga wa kutosha, uwazi na madirisha makubwa yenye kuruhusu hewa kuingia na kutoka katika pande zote. Ina veranda pana mbele ya kila wodi na katikati ya majengo kuna nafasi kubwa yenye nyasi zinazopunguzwa vizuri kila mara. Kwa upande mwingine mpangilio wake wa utendaji kazi unashabihiana sana kimantiki na ule wa Ulaya.

Mawodi hufikika kupitia veranda hii

Jengo zima la hospitali limejengwa usawa wa ardhi isipokuwa majengo mawili yenye ghorofa moja yaliyounganishwa katika miisho miwili ya jengo kuu lenye veranda pana iliyoezekwa na iliyo wazi sehemu zote.

Mlango wa kuingilia upo katika jengo la mbele lililojengwa usawa wa ardhi. Ofisi za utawala na ile ya mkurugenzi wa hospitali zipo katika gorofa ya kwanza. Katika jengo lililoko nyuma kuna jiko, maktaba, duka la madawa, kikanisa kidogo cha hospitali na ofisi za utawala wa chuo kikuu. Misingi ya jengo zima la hospitali ni mirefu kiasi cha nusu meta zaidi ya eneo lenye nyasi zinazofyekwa vizuri mara kwa mara, hii ni kukinga jengo dhidi ya mafuriko wakati wa masika na pia wakati wa mvua zenye ngurumo kali. Mwisho, njia zote zinazounganisha majengo zimeezekwa.

Kwenye wodi kuna vyumba vikubwa kwaajili ya wagonjwa 40 na pia vyumba vidogo

Idara

Hospitali ya Mt. Fransisko ina vitanda 371, na imegawanyika katika idara za upasuaji,utaalam wa magonjwa ya ndani,magonjwa ya akina mama na uzazi, magonjwa ya watoto, magonjwa sugu na chumba cha wagonjwa mahututi. Pia kuna idara za wagonjwa wanaofika kutibiwa wakitokea majumbani kwao, wodi za kifua kikuu, tiba ya meno, mazoezi ya viungo vya mwili, magonjwa ya akili, ukoma, chumba cha urejeshwaji wa utendaji kazi wa viungo, mazoezi na viungo bandia, idara ya x-ray na maabara. Pia maabara maalum kwaajili ya uzalishaji wa maji ya kutundikia wagonjwa, jambo ambalo Ulaya haliwezi kufikirika.
Wagonjwa wanaofika kutibiwa wakitokea majumbani kwao hufanyiwa uchunguzi na kutibiwa katika jengo maalum lililopo mbele ya hospitali, lenye idara za magonjwa ya macho, ngozi na Ukimwi ( AIDS)

Idadi ya wagonjwa ni kubwa sana

Jumla ya wagonjwa 100,000 hutibiwa kwa mwaka katika idara ya wagonjwa wanaotibiwa na kurejea majumbani kwao, na wastani wa wagonjwa 17000 hulazwa kila mwaka. Idadi ya watoto wanaozaliwa kila mwaka hufikia 5000.

Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na idadi yaUongozi wa hospitali

Hospitali inaendeshwa na kamati maalum maarufu kama „Board of Governors“ Nusu ya wawakilishi ni kutoka katika jimbo la Mahenge ya Ifakara na sehemu nyingine ni wawakilishi kutoka serikalini. Askofu Libena ni mwenyekiti wa kamati.

Askofu Salutaris Libena Shughuli za kila siku huendeshwa na kamati yenye watu 3 Dr. Fr. Winfried Gingo - mganga mkuu Mr. Onesmo Ngenzi - Mkurugenzi Mr. Meshak Lubuleje - Patroni

Taarifa zaidi.....

Fedha:

Hospitali ina ufadhili wa aina mbili; serikali ya Tanzania na Jimbo katholiki Ifakara. Gharama za uendeshaji, kama mishahara na madawa hutolewa na serikali. Ukarabati wa majengo na matumizi kama vile ununuzi wa vifaa vipya na marupurupu ya wafanyakazi hugharimiwa na Jimbo. Chanzo muhimu cha fedha ni michango ya matibabu itolewayo na wagonjwa kwaajili ya malazi, madawa na matibabu. Kiasi hiki hufanya 36% ya chanzo kizima cha pesa. Hata hivyo walio masikini kabisa hupata msamaha. Kinadharia, mwenendo huu wa uchumi waonekana kuwa wenye mantiki; ila kwa bahati mbaya hauendani na hali halisi hata kidogo.

Matatizo makubwa.......

powered by webEdition CMS